Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RC Tabora Awataka Wafanyabiashara Mkoani Humo Kuwa Mstari wa Mbele Katika Uwekezaji
Oct 26, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37438" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wakazi wa Tabora na hasa wafanyabiashara na Wajasiriamali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(hayupo katika picha) wakati akiwatangazia jana juu ya Jukwaa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika mwishoni mwa Mwezi Novemba mwaka huu.[/caption]

Na: Tiganya Vincent, RS TABORA

 

Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kutumia kikamilifu Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lijalo mkoani humo kutangaza fursa za biashara na uwekezaji ili waweze kuinua na kupanua wigo na mitaji yao.

 

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wa hadhara uliolenga kuwatangazia wananchi, wafanyabiashara  na Wajasiriamali wa Mkoa juu ya Jukwaa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.

 

[caption id="attachment_37440" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya akizungumza na wananchi jana katika soko kuu juu ya maandalizi ya kushiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika mwishoni mwa Mwezi Novemba mwaka huu.[/caption]

Alisema Jukwaa hilo ni fursa nzuri kwa wakazi wa Tabora na hasa wafanyabiashara  na Wajasiriamali kuongeza mtandao wa biashara kati yao na wale wa kutoka nje ya Mkoa huo kupitia utangazaji wa bidhaa zao na fursa zilizopo za uwekezaji.

 

Mwanri alisema hatua hiyo itawasaidia kuwafanya kuwa wachangia katika fursa za uwekezaji  na biashara mkoani humo na sio kuwaacha kama watazamaji wa watu kutoka nje kuja kunufaika pekee yao.

 

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wamiliki wa Hoteli na Nyumba za kulala wageni , Madereva bodaboda na vyombo vingine vya usafiri kuhakikisha wanakuwa wakarimu na kutoa huduma ambayo itawafanya washiriki wa Jukwaa hilo watamani kuwekeza Tabora.

 

[caption id="attachment_37441" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na wananchi jana katika soko kuu juu ya maandalizi ya kushiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika mwishoni mwa Mwezi Novemba mwaka huu.[/caption] [caption id="attachment_37442" align="aligncenter" width="750"] Naibu Meya wa Manispaa ya Tabora Yahaya Muhamali akizungumza na wananchi jana katika soko kuu juu ya maandalizi ya kushiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika mwishoni mwa Mwezi Novemba mwaka huu na kuvitaka vikundi vya wanawake, vijana na walemavu kwenda kuchukua mkopo.[/caption]

Alisema wananchi wa Tabora wanatakiwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo kuwafichua waharifu ili kuweka mazingira mazuri ambayo yatawafanya watu wenye nia ya kuwekeza kuwa na uhakika wa usalama wa uwekezaji wao.

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya aliwataka watu wenye nia ya kuwekeza kwenda Tabora kwa sababu ya kufunguka kwa miundombinu muhimu ya kuvutia ikiwemo  barabara za lami zinaunganisha Mkoa huo na mingine, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria na Uwanja wa Ndege unaoruhusu ndege kubwa kutua masaa 24.

 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema katika kuhakikisha Manispaa ya Tabora inaendelea kuwa mahali salama pa kuwekeza ameliagiza Jeshi la Polisi kuendesha Doria la kukapambana na majambazi , vibaka na waharifu wengine.

 

Alisema lengo ni kuhakikisha Tabora inakuwa sehemu mfanyabiashara ataendesha shughuli zake bila hofu na mashaka ya kuvamiwa.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi