Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RC Mongella Aipongeza Mamlaka ya Maji Mwanza
Oct 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36196" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) alipowasili kwenye ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka, Mhandisi Anthony Sanga (kulia).[/caption]

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) kwa kubuni na kuendeleza Mfumo wa Upimaji wa Utendaji wa watumishi wake Kikanda ambao alisema unaleta ufanisi wenye tija.

Pongezi hizo alizitoa Oktoba 01, 2018 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka hiyo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa watumishi wa Kanda ya Makongoro ambayo ilishinda vigezo vinavyotumika kupima utendaji wa watumishi kikanda ambavyo ni mauzo na makusanyo.

Mfumo huo wa upimaji wa utendaji kwa watumishi wa MWAUWASA ulizinduliwa rasmi Agosti mwaka huu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ambao unapima utendaji wa watumishi kikanda kupitia kanda zake mbazo ni Makongoro, Nyegezi, Nyakato na Kanda ya Mjini Kati.

Katika mashindano hayo kwa mwezi Septemba, 2018 Kanda iliyoongoza ni Makongoro kwa kupata asilimia 96.35 ikifuatiwa na Kanda ya Mjini Kati asilimia 96.07, Kanda ya Nyegezi asilimia 95.36 na mwisho ni Kanda ya Nyakato asilimia 94.99.

[caption id="attachment_36195" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya MWAUWASA, Christopher Gachuma (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa watumishi wa Kanda ya Makongoro ambayo ilishinda vigezo vinavyotumika kupima utendaji wa watumishi kikanda ambavyo ni mauzo na makusanyo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.[/caption]

“Pongezi kwenu Bodi, Menejimenti na Watumishi wa MWAUWASA kwa kubuni huu mfumo wa kushindana ambao na wengine wanapaswa kuiga ili kupiga hatua,” alisema.

Mongella alisema kwa namna ambavyo Mamlaka hiyo inavyoendesha shughuli zake ni dhahiri kwamba itaendelea kuwa kinara miongoni mwa Mamlaka za Maji nchini kwa utendaji bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya MWAUWASA, Christopher Gachuma alipongeza umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi na aliwataka waendeleze hayo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Gachuma alisema mafanikio yanayoonyeshwa na Mamlaka hiyo ni kutokana na uongozi thabiti na mahiri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka sambamba na mshikamano uliyopo miongoni mwa watendaji na aliwaasa kuhakikisha wanauendeleza na kuuzidisha kila inapobidi.

[caption id="attachment_36197" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa watumishi wa Kanda ya Makongoro iliyoshinda kiutendaji. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya MWAUWASA, Christopher Gachuma na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Anthony Sanga. Kulia kwake ni Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka, Edith Mudogo na Denisa Pagula.[/caption]

Akizungumzia vigezo vilivyotumika kupata mshindi wa kanda iliyofanya vizuri kwa Mwezi Septemba, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Anthony Sanga alivitaja kuwa ni mauzo na makusanyo.

Hata hivyo alibainisha kuwa vigezo vya kupima utendaji vitaongezwa kutoka viwili hadi vitano ambavyo kwa ujumla wake alivitaja kuwa ni mauzo, makusanyo, maunganisho mapya ya wateja, uharaka wa kutatua malalamiko ya wateja hususan suala zima la upatikanaji wa maji na udhibiti wa upotevu wa maji kwa kiwango kinachokubalika.

Mhandisi Sanga alisema kwamba lengo kubwa la mfumo huo ni kuongeza makusanyo, kuongeza mauzo ya maji lakini pia kuhakikisha maji yanafika kila kona ya jiji la Mwanza na viunga vyake kwa maana ya usambazaji wa maji, kupunguza upotevu wa maji sambamba na kuhakikisha wateja wote wanaunganishwa kwenye mfumo wa maji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi