Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Azindua Mradi na Kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kisasa wa Michezo
Jun 03, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akindoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Mradi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Kisasa wa Michezo “Zanzibar International Criket Club and Sports Complex” Fumba Zanzibar , akiwa na Mwakilishi wa Kampuni ya JHIL Enterprises kutoka India Bw. Sunil Manohar Gavaskar, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika katika eneo la ujenzi wa mradi huo Fumba Wilaya ya Magharibi”B” Unguja leo 3-6-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza wa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya JHIL Enterprises ya India, Bw. Jilesh Hitmat Babla, (kushoto kwa Rais) akitoa maelezo ya ramani ya michoro ya ujenzi wa Uwanja wa Criket wa Kisasa katika eneo la Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati wa uzinduzi wa mradi huo na Uwekaji wa Jiwe la Msingi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita
Wananchi wa Kijiji cha Fumba waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Mradi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Mradi wa Kisasa wa Michezo “Zanzibar International Criket Club and Sports Complex” unaojengwa katika eneo la maeneo huru ya Uchumi Fumba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika katika eneo la mradi huo Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-6-2022.