Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Waziri) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrisa Andulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kaulimbiu “Wajibu wa Mahakama na Wadau wa Sheria kwa Kuendena na Kasi ya Awamu ya Nane Kushughulikia Kesi”.
Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.