Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpatia picha na vitabu vya Kiswahili mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema na baadae kukabidhi zawadi hizo katika ziara yake ya siku moja nchini kabla ya kuanza mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanahabari katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.