Rais Mhe.Samia Ashiriki Kumbukizi ya Mwaka Mmoja wa Hayati Dkt. Magufuli Chato
Mar 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Wananchi wa Chato pamoja na Wageni kutoka Sehemu mbalimbali nchini katika Kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika uwanja wa Michezo wa Magufuli leo tarehe 17 Machi, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Philip Mpango akiambatana na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango, leo tarehe 17 Machi 2022 ameshiriki Kumbukizi ya Mwaka Mmoja wa Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli , iliofanyika Chato mkoani Geita.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiweka Shada la Maua katika kaburi la Hayati John Pombe Magufuli, baada ya kumalizika kwa Ibaada ya Kumbukizi ya Mwaka Mmoja wa Hayati Magufuli iliyofanyika katika Uwanja wa Magufuli Chato Mkoani Geita.