Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata Utepe kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Othman Makungu wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa Dodoma, Mhe. Antoni Mtaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu sehemu ya uendeshaji Haki mara baada ya kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai.