Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni Pre & Primary School iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akimkabidhi mfano wa funguo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kama ishara ya makabidhiano ya Shule hiyo ya Awali mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika Shule hiyo ya Museveni Pre & Primary School Chato mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakikagua baadhi ya majengo ya Shule hiyo ya Awali na Msingi iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Chato mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021 mara baada ya kuizindua rasmi Shule hiyo.