Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Azungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC)
Dec 02, 2025
Rais Samia Azungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC, Mhe. Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC), Mhe. Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025. Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira. Aidha, Lord Swire ameomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC), Mhe. Lord Hugo Swire mara baada ya mazungumzo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi