Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Azindua Ugawaji wa Vizimba vya Kufugia Samaki na Boti za Kisasa Jijini Mwanza
Jan 30, 2024
Rais Samia Azindua Ugawaji wa Vizimba vya Kufugia Samaki na Boti za Kisasa Jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia samaki na boti za kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega kuhusu boti za kisasa na vizimba vya kufugia samaki kwa ajili ya wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa ziwa Victoria (Bismarck Rock) jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi mfano wa funguo wawakilishi wa vikundi vya uvuvi kwa ajili ya ugawaji wa vizimba vya kufugia samaki na boti za kisasa kwa ajili ya wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa ziwa Victoria (Bismarck Rock) jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia samaki na boti za kisasa kwa ajili ya wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa ziwa Victoria (Bismarck Rock) jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Muonekano wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia samaki ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua ugawaji wake kwa ajili ya wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Boti na vizimba hivyo vimegawiwa kwa wavuvi kwa mkopo usio na riba ili kuwawezesha kufanya biashara ya samaki kwa tija.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi