Rais Samia Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya BRT II, Azindua Mradi wa Maboresho ya Miundombinu ya Bandari ya Gati namba 0-7
Dec 05, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Wengine katika picha ni Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya Barabara ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa mkoani Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi Rasmi kwa ajili ya matumizi ya mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika Bandarini Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Eric Hamissi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kufungua rasmi kwa ajili ya matumizi ya mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Eric Hamissi kuhusu Ujenzi wa gati namba 0 hadi 7 kabla ya kuzindua rasmi kwa ajili ya matumizi katika hafla iliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.