Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Awawezesha Wachimbaji Wadogo wa Madini
Mar 04, 2025
Rais Samia Awawezesha Wachimbaji Wadogo wa Madini
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa tume hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita tarehe 4 Machi, 2025 katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO Dodoma.
Na Frank Mvungi

Wachimbaji wadogo nchini wametajwa kunufaika na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka minne.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 4, 2024 jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Tume ya Madini, Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema Serikali imefanikiwa kutenga maeneo 58 kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika mikoa mbalimbali nchini.

"Tume imeweka mazingira rafiki kwa ajili ya wachimbaji wadogo kupata leseni za uchimbaji pamoja na kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili wapate mikopo kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za uchimbaji", alisisitiza mhandisi Lwamo.

akifafanua Mhandisi Lwamo amesema Tume itaendelea  kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Kuhusu Leseni zilizotolewa na Tume Mhandisi Lwamo  amesema jumla ya leseni 41,424 kati ya 37,318 zilizopangwa kutolewa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Serikali ya Awamu ya Sita.

" Kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mauzo ya madini katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini yameendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2,361.80 hadi shilingi bilioni 2,597.18 kwa mwaka 2023/2024", alisema Lwamo.

Mhandisi Lwamo amesema kuwa ukuaji wa sekta ya madini unatarajiwa kufikia asilimia 10 na zaidi ifikapo mwaka 2025.

Aidha, Mhandisi Lwamo amesema kuwa ajira 19,874 zimezalishwa na makampuni ya uchimbaji ambapo kazi ya hizo 19,371 ni watanzania.

Sekta ya madini ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi