Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima
Dec 28, 2023
Rais Samia Atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Desemba 28, 2023 ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Usimamizi wa Utalii na Masoko (Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing (Honoris Causa)) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) visiwani Zanzibar. Ametunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa chuo hicho, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Na Mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Desemba 28, 2023 ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Usimamizi wa Utalii na Masoko (Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing (Honoris Causa)) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) visiwani Zanzibar.

Ametunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuimarisha utalii na kuchochea ukuaji wa uchumi. 

Hii ni shahada ya tatu kutunukiwa ambapo nyingine ni Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) ya Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha nchini India na Shahada ya Udaktari wa Heshima ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi