Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Atunukiwa Medali na Umoja wa Falme za Kiarabu
May 06, 2025
Rais Samia Atunukiwa Medali na Umoja wa Falme za Kiarabu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Medali ya Mother of the Nation Order na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025. Medali hiyo imetoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Medali ya  Mother of the Nation Order kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan. Medali hiyo iliwasilishwa kwake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.

Medali hiyo ni moja kati  ya Medali za juu kabisa kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).  Medali hiyo hutolewa kutambua mchango wa kiongozi katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yake.

Serikali ya UAE imetambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu ambayo yanaendana na Sera  za UAE za maendeleo endelevu katika jamii, uwezeshaji wanawake na ushirikiano wa kimataifa.

Sheikh Abdullah aliwasilisha salamu kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na kuwatakia kheri wananchi wa Tanzania katika maendeleo pamoja na ustawi zaidi. Pia alisisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa kudumu baina ya nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa kupanua ushirikiano katika sekta muhimu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi