Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Atamani Kuona Wananchi Wengi Wakijihusisha na Uvuvi
Jan 30, 2024
Rais Samia Atamani Kuona Wananchi Wengi Wakijihusisha na Uvuvi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Na Ahmed Sagaff - Maelezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema anatamani kuona idadi ya wananchi wanaojihusisha na uvuvi inaongezeka ili kukuza sekta hiyo na kuwanufaisha wananchi.

Akizungumza leo jijini Mwanza, Rais Samia ameeleza kuwa serikali inafanya mageuzi makubwa katika sekta ya uvuvi.

"Kwa mujibu wa takwimu tulizonazo, Tanzania ina wavuvi takriban 197,763 na wakuzaji wa viumbemaji 34,057. Aidha mnyororo mzima wa uvuvi umeajiri karibu watu milioni sita ambapo idadi ni kubwa lakini tuna haja ya kuongeza idadi ya walioajiriwa," ameeleza Mheshimiwa Rais.

Pamoja na hilo, Rais Samia amefahamisha kuwa serikali imechukua hatua za awali za kukuza sekta ya uvuvi ni kuimarisha wizara ya mifugo na uvuvi ili iweze kuendana na dhamira ya uvuvi wa kisasa.

Tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 Rais Samia amekuwa akitoa matamko mbalimbali ya kuwataka watumishi wa sekta ya uvuvi kuongeza ufanisi huku akiwasisitiza wananchi kujiajiri katika sekta hiyo kwa faida ya maisha yao binafsi na kuinua uchumi wa Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi