Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Ashuhudia Utiaji Saini Makubaliano ya Ushirikiano wa Pamoja katika Sekta mbalimbali.
Jun 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Waziri wa Nishati January Makamba wakati akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye masuala ya Nishati (Oil and Gas) kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana akibadilishana Mkataba wa Makubaliano kwenye masuala ya Utalii kupitia Wizara ya Urithi na Utalii ya Oman (kwenye Sekta ya Utalii) ya nchi hiyo.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye Sekta ya Elimu ya Juu pamoja na Serikali ya Oman

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Shariff Ali Shariff akisaini Mkataba wa Makubaliano pamoja na Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Oman (OIA) kuhusu Mashirikiano ya kutangaza Uwekezaji baina ya nchi mbili kushirikiana katika kupata uzoefu

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi