Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Ashiriki kwenye Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Apr 10, 2024
Rais Samia Ashiriki kwenye Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Baraza la Eid El Fitr ambalo Kitaifa limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2024.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni mbalimbali pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Baraza la Eid El Fitr ambalo Kitaifa limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu, Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally wakati wa Baraza la Eid El Fitr ambalo Kitaifa limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA), Mama Shamim Khan wakati wa Baraza la Eid El Fitr ambalo Kitaifa limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu, Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Omar pamoja na Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA), Mama Shamim Khan mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Baraza la Eid El Fitr tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA), Mama Shamim Khan ambaye aliwasilisha kwa niaba ya Wanajumuiya wenzake wakati wa Baraza la Eid El Fitr lililofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2024.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi