Rais Samia Apokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan
Apr 18, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Na
Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ikulu ya KulliyeAnkara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya KulliyeAnkara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Kushoto ni Mwenyeji wake Rais wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya KulliyeAnkara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.