Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Apokea Hundi ya Zaidi ya Bilioni 2 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali
Dec 10, 2023
Rais Samia Apokea Hundi ya Zaidi ya Bilioni 2  kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya shilingi bilioni mbili kutoka kwa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu kwa ajili ya maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika Mji Mdogo wa Katesh, Hanang mkoani Manyara hivi karibuni. Hundi hiyo ni michango iliyochangwa na Taasisi mbalimbali za Serikali na kuwasilishwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023 mara baada ya kupokea hundi ya michango kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika Mji mdogo wa Katesh, Hanang Mkoani Manyara hivi karibuni. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023. 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi