Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Aongoza Kuaga Mwili wa Hayati Ali Hassan mwinyi
Mar 02, 2024
Rais Samia Aongoza Kuaga Mwili wa Hayati Ali Hassan mwinyi
Gari Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa limebeba mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan Mwinyi likipita katika barabara ya Amani kuelekea katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa viongozi wa Kitaifa na wananchi wa Zanzibar.
Na Ikulu - Zanzibar

Wajane wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan Mwinyi, Mama Khadija Mwinyi   (kulia) na Mama Siti Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kwa ajili ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan, hafla hiyo iliyofanyika leo 2-3-2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakitoa heshima za mwisho kwa Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania,  hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya New Amaan Complex Amaan Zanzibar leo 2-3-2024.
Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyii akisalimiana na kuagana na Makamu wa Rais wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi  Ndaitwah, baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Rais wa Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan Mwinyi, hafla hiyo iliyofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex  Zanzibar leo 2-3-2024.
Viongozi wastaafu wakitoa heshima za mwisho kwa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar leo 2-3-2024.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi