Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Ujumbe wa TLS na TAWJA
Aug 12, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ulioongozwa na Rais wa Chama hicho, Profesa Edward Hoseah, wakati Ujumbe huo ulipofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 11 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Joaquine De-Mello, wakati alipoongoza Ujumbe wa Chama hicho, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 11 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Jaji Joaquine De-Mello, wakati Ujumbe huo ulipofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 11 Agosti, 2021.