Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Uswis, Awasili Jijini Dar es salaam
Nov 26, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uswisi ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bi. Patricia Danzi kushoto, wakati ujumbe huo ulipofika Jijini Dodoma leo tarehe 26 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Dodoma leo tarehe 26 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Dodoma leo tarehe 26 Novemba, 2021.