Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Stephen Mbundi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Aprili 13, 2026 yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa nchi wanachama.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kukuza mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo.