Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Aihimiza Jamii Kupanda Miti Kukabiliana na Tabianchi
Nov 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na mwandishi wetu , Manyara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameihimiza jamii kupanda miti ya kutosha lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ambayo yameanza kuleta athari katika mazingira.

Mhe. Samia amesema hayo leo Novemba 23, 2022 katika Mkutano wa Hadhara na Wananchi wa Babati mkoani Manyara uliofanyika katika Uwanja wa Kwaraa, ambapo amesema jamii inapaswa kuacha kukata miti na badala yake wapande miti kwa wingi katika maeneo mbalimbali.

"Nawaasa kupunguza migogoro baina yenu hasa migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo inaharibu taswira ya nchi yetu, nawasihi pia wanasiasa kuacha tabia ya kuchochea migogoro hiyo bali kuwa mstari wa mbele kusimamia mipango bora ya matumizi bora ya ardhi", amesema Mhe. Samia.

Amewaasa Watanzania kuacha tabia ya ukakitili wa kijinsia, akitolea mfano Mkoa wa Manyara kuwa na Idadi kubwa ya matukio ya ukatili wa kijinsia ambapo amesema katika ripoti ya mwaka jana ilionesha jumla ya matukio 3641, ambapo Mkoa huo ulikuwa na matukio 792 yaliyohusisha mashambulio ya kimwili na matukio 708 yakihusisha unyanyasaji wa watoto kingono.

Mhe. Samia ametumia nafasi hiyo kuwaasa wakulima kujisajili katika Wilaya zao ili watambulike na wapate huduma sahihi kulingana na mahitaji yao katika maeneo yao lengo likiwa ni kuongeza tija katika Sekta ya kilimo.

Amesema kuwa, Watanzania hawana sababu ya kulalamika njaa kwa kuwa Serikali inaboresha mazingira ya kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji, ambapo amehimiza Watanzania kulima na kuhifadhi chakula.

Aidha, Mhe. Samia amewahimiza Wananchi kulipia huduma pale wanapohitajika kufanya hivyo ili Serikali iweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi, vile vile amehimiza Watanzania kuendelea kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi