Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji, Hayati William Tate Ole Nasha wakati wa kuaga mwili wa Naibu Waziri huyo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Sept 30,2021.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kazi kubwa anayoifanya katika kujenga Taifa la Tanzania, kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Taarifa ya Kielektroniki ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’s kwa maendeleo ya Taifa katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Taarifa ya Kielektroniki ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’s kwa maendeleo ya Taifa katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kazi za Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) alipotembelea mabanda ya maonesho katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.