Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Maji App itakayowezesha kupatikana kwa taarifa za utekelezeaji wa miradi ya maji katika Mikoa,Wilaya na vijiji mbalimbali nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Taarifa ya mwaka ya Utendaji Kazi wa Mamlaka za maji na mazingira mijini kabla ya kuzungumza na viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Maji iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Mhandisi Judith Odunga kwa niaba ya Chama cha Wahandisi Wanawake Tanzania ya kutambua mchango wake katika utendaji wake wa kazi kwenye sekta ya maji nchini.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliohudhuria maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Maji iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Machi, 2022.