Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Ahudhuria Mazishi ya Kitaifa ya Dkt. Hage Geingob
Feb 25, 2024
Rais Samia Ahudhuria Mazishi ya Kitaifa ya Dkt. Hage Geingob
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu, Dkt. Hage Geingob katika uwanja wa Michezo wa Uhuru jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024. Hayati Rais Geingob alifariki dunia tarehe 04 Februari na anatarajiwa kuzikwa tarehe 25 Februari, 2024 katika Makaburi ya Mashujaa ya Heroes’ Acre Jijini Windhoek
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Namibia, Marehemu Dkt. Hage Geingob kwenye uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024. Hayati Rais Geingob alifariki dunia tarehe 04 Februari na anatarajiwa kuzikwa tarehe 25 Februari, 2024 katika Makaburi ya Mashujaa ya Heroes’ Acre jijini Windhoek

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Monica Geingos mara baada ya kuzungumza na kutoa heshima za mwisho katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Namibia, Marehemu Dkt. Hage Geingob kwenye uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi