Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Ahudhuria Hafla Uzinduzi Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Makao Makuu ya AU
Feb 18, 2024
Rais Samia Ahudhuria Hafla Uzinduzi Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Makao Makuu ya AU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wakati wakielekea kwenye hafla ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshika utepe pamoja na viongozi mbalimbali wakati Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema akikata utepe huo kuashiria uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali katika uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024.

 

Taswira ya Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyowekwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa kwa ajili ya kutambua mchango wake katika masuala ya ukombozi Barani Afrika tarehe 18 Februari, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi