Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne nchini Ethiopia kwa kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Februari 14 na 15, 2026.
Katika mkutano huo, Rais Samia alijumuika na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kujadili masuala ya maendeleo ya bara, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kushughulikia changamoto zinazoikabili Afrika.

Mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi, alikutana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Innocent Shiyo, pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo na kuwapongeza kwa kuendelea kuiwakilisha vyema Tanzania na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ethiopia.

.
Aidha, Rais Samia alikutana na viongozi wa Diaspora na Watanzania wanaoishi nchini Ethiopia akiwasisitiza umuhimu wao katika kuchangia maendeleo ya Taifa wakiwa nje ya nchi.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Tanzania kuendelea kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kimataifa na kuimarisha nafasi yake ndani ya Umoja wa Afrika