Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Gran Meliá kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.
Viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa kwenye ukumbi wa Hoteli ya Gran Meliá kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wastaafu kutoka Afrika mara baada ya kufungua Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika katika hoteli ya Gran Meliá Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.