Rais Samia Afunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Uhamiaji kozi Na.1/2022
Aug 15, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Salaam na Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipanda mti mbele ya Jengo la Ofisi za Chuo cha Jeshi la Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, alipowasili Chuoni hapo kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari 820 wa Jeshi la Uhamiaji tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti kwa Mshindi wa Jumla kwenye Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji, Konstebo Geofrey Felician Zakaria, wakati wa Ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya Wahitimu 818 katika Chuo cha Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni kabla ya kufungua Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji katika Hafla iliyofanyika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.