Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Mwinyi Azungumza na CDF Mkunda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na Uongozi wa Benki ya TCB
Jan 13, 2024
Rais Mwinyi Azungumza na CDF Mkunda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na Uongozi wa Benki ya TCB
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kumpongeza kwa Maadhimisho ya Kilele cha Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Complex Zanzibar jana 12-1-2024, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 13-1-224.
Na Ikulu - Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mgeni wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar  leo 13-1-2024.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Stephen Mbundi alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo 13-1-2024 na (kulia kwake) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Mhe. Balozi Said Shaib Mussa.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar ulioongozwa na Mjumbe wa Bodi wa Benki hiyo, Dkt. Issack Allan (kulia kwa Rais) akimuwakilisha Mwenyeki Bodi ya Benki hiyo na (kushoto kwa Rais) ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Ndg. Juma Malik Akili, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kijitambulisha leo 13-1-2024.

 

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi