Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Mhe. Suluhu Azungumza na Wake wa Viongozi Mbalimbali Ikulu Tunguu Zanzibar
Mar 09, 2022
Na Jacquiline Mrisho


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wake wa Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 08 Machi, 2022 Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mke wa Makamu wa Rais Mbonimpaye Mpango, Mke wa Rais wa Zanzibar Mariam Mwinyi pamoja na Wake wa viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuzungumza nao katika hafla fupi iliyofanyika katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Wake wa Viongozi mara baada ya kuzungumza nao katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022

Sehemu ya Baadhi ya Wake za Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla fupi iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022 iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar.

Sehemu ya Baadhi ya Wake za Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla fupi iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022 iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi katika picha ya kumbukumbu pamoja na Waandaaji wa Filamu ya Kitanzania ya Binti.  Seko Shamte wa kwanza (Kushoto) ni Mtayarishaji/Producer wa filamu hiyo pamoja na Godliver Gordian muigizaji mkuu katika Filamu hiyo ambayo inaoneshwa na mtandao maarufu wa Marekani wa kutazama filamu na vipindi vya runinga kupitia Mtandao (Netflix)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango (kulia) pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi