Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Azindua Nembo na tarehe ya Sensa ya Watu na Makazi
Apr 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Sensa, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo rasmi wakati wa uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. John Jingu, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Hessein Ali Mwinyi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua rasmi Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika rasmi, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SC Johnson ya nchini Marekani, Bw. Fisk Johnson Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SC Johnson ya nchini Marekani, Bw. Fisk Johnson na Ujumbe wake baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.