Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Awaapisha Viongozi Mbalimbali Ikulu Chamwino Jijini Dodoma
Apr 02, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Pindi Hazara Chana kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Jaji Mstaafu Ibrahim Mipawa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili, 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Peter Ilomo kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Suzan Mlawi kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 02 Aprili 2022.
Viongozi walioapishwa Wakila Kiapo cha Maadili, kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili, Jaji Sivangilwa Mwangesi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Mawaziri pamoja na Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Spika wa Bunge, Mhe. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Mhe. George Boniface Simbachawene, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Damas Daniel Ndumbaro pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Pindi Hazara Chana mara baada ya hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili, 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Spika wa Bunge, Mhe. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji Mstaafu Ibrahim Mipawa, Peter Ilomo Mjumbe wa Baraza la Maadili na Suzan Mlawi Mjumbe wa Baraza la Maadili, kwenye hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.