Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Apokea Taarifa ya TAKUKURU na CAG kwa mwaka 2020/2021, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma
Mar 30, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Taasisi ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, CP Salum Hamduni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uwasilishwaji wa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022.