Rais Mhe. Samia Azungumza na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50 Alain Ebobisse, Azindua Nyumba 644 za Magomeni Kota
Mar 23, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50, Alain Ebobisse mara baada ya mazungumzo yao Ikulu mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Msanifu majengo Daud Kondoro wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali za Ujenzi wa Nyumba 644 katika eneo la Magomeni Kota mkoani Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi mfano wa Ufunguo kwa Bibi Mwajuma Sama na Mzee Henry Ngwemba kama ishara ya kuwakabidhi Nyumba mara baada ya kuzindua rasmi mradi wa Nyumba 644 Magomeni Kota mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi 2022.