Rais Mhe. Samia Azungumza na Mkurugenzi wa UN Women Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, Amsalimia Mama Fatma Karume, Awafariji Waliopotelewa na Watoto kwenye Ajali ya Ndege
Mar 09, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa UN Women Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Maxime Houinato na Ujumbe wake mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Tunguu Zanzibar leo tarehe 09 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mama Fatma Karume alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja leo tarehe 09 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Sadala Mabodi na familia yake, alipomtembelea nyumbani kwake Chukwani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo tarehe 09 Machi, 2022 kwa ajili ya kumfariji kutokana na kupotelewa na Mtoto wake kwenye ajali ya Ndege.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Sadala Mabodi na familia yake, alipomtembelea nyumbani kwake Chukwani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo tarehe 09 Machi, 2022 kwa ajili ya kumfariji kutokana na kupotelewa na Mtoto wake kwenye ajali ya Ndege.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na familia ya Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Ahmed Nassor Mazrui alipowatembelea nyumbani kwao Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo tarehe 09 Machi, 2022 kwa ajili ya kuwafariji kutokana na kupotelewa na Mtoto wao kwenye ajali ya Ndege.