Rais Mhe. Samia Amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi
Mar 15, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Waziri Kindamba Waziri akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi. Humphrey Polepole wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba mara baada ya hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.