Rais Mhe. Samia Amuapisha Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Ikulu Jijini Dar es Salaam
Jun 30, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (Chief of Defense Forces-CDF), Jenerali Jacob John Mkunda katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Luteni Jenerali Salum Haji Othman kabla ya kumuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff -C of S) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Luteni Jenerali Salum Haji Othman kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff -C of S) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio la Uapisho wa Mkuu wa Majeshi pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lililofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (Chief of Defense Forces-CDF) Jenerali Jacob John Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff -C of S) Luteni Jenerali Salum Haji Othman katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022.