Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli – Tunaibadilisha Dar-es-Salaam, Tunaipendezesha Dar-es-salaam
Sep 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Judith Mhina- MAELEZO

  • Azindua Flyover ya Mfugale TAZARA
  • Kujenga Flyover makutano ya Changombe , Uhasibu, Gerezani na Morroco /Mwenge
  • Ubungo Interchange ya ghorofa tatu
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezindua barabara ya juu ya Mfugale Flyover ambayo imeleta faraja kubwa kwa Watanzania kuwa na sisi tunaweza pia, imebadili manthari ya Jiji la DAR-ES-SALAAM.

Akizindua Daraja la Mfugale Rais Magufuli amesema “Daraja hii imebadili historia ya nchi yetu kwa kuwa ni flyover ya kwanza tangu tupate Uhuru, na imegharimu fedha za Tanzania Bilioni 106.965”.

Pia imeondoa Changamoto kubwa ya foleni iliyowakumba wakazi wa Dar-es-salaam kama wafanyakazi, wafanyabiashara, wasafiri wa ndege na wakazi wa maeneo ya Gongo la Mboto, Chanika, Kisarawe  na vitongoji vyake.

Aidha, kutokana na foleni hizo za Mkoa wa Dar-es-salaam, zimeathiri shughuli za kiuchumi na maendeleo pia, kupoteza takribani fedha za Tanzania Bilioni 400 kila mwaka. Vilevile foleni hizo zimeleta adha za kijamii kama vile Wazazi kuchelewa kurudi nyumbani na kuathiri baadhi ya familia.

Akitoa hali halisi la Jiji la Dar-es-salaam litakavyokuwa baada ya miaka michache ijayo Rais amesema jumla ya barabara za juu 4 zitajengwa katika makutano ya Changombe au ali maarufu machinjioni Gerezani, Morocco/Mwenge na Ubungo interchange itakayokupa ya ghorofa tatu, ambayo itagharimu fedha za Tanzania Bilioni 247.

Kama hiyo haitoshi, Rais Magufuli ameongeza barabara ya Kimara mpaka Kibaha itakuwa na barabara sita yaani tatu upande wa kuingia na tatu kutoka Mkoa wa Dar-es-salaam. Aidha barabara hii itasaidiwa na barabara pembezoni pande zote mbili, hivyo itakuwa na jumla ya barabara 8 itakayokuwa na urefu wa kilometa 19.2.

“Lengo letu ni kulibadilisha Dar-es-salaam, kuipendezesha Dar-es-salaam. Dar es-salaam itabadilika”

Akitoa sababu ya daraja kuitwa jina la Mhandisi Patrick Aron Mfugale Rais amesema kuwa, ni kutokana na uzalendo aliouonyesha katika kuwajibika na kuwa na matumizi mazuri ya fedha za umma, pamoja na utaalamu wake uliotukuka katika ujenzi wa madaraja. Pia, tangu aanze kazi mwaka 1977 amepitia Changamoto nyingi za kiutendaji ambazo alizikabili na kusonga mbele.

“Binafsi nampongeza sana Mhandisi Patrick Mfugale ambaye ni mchapa kazi mzalendo mbunifu muadilifu na mwaminifu. Akielezea baadhi ya Changamoto alizozipata miaka 1984 akiwa anafanya kazi kwa watani zangu kule Songea Matomondo na Kimasela wakati wa kujipumzisha katika kibanda walichojenga walikuwa wakilala kesho yake saa nne walijikuta wako nje”.

Akifafanua utendaji uliotukuka wa Mhandisi Mfugale Rais amesema “Mfugale ni kiongozi ambaye amesimamia madaraja makubwa kama vile madaraja ya Mkapa la kilometa 10 Umoja, Kikwete, (Maragarasi)

Mwaka 2006 alipewa tunzo na Rais Benjamin William Mkapa kama mfanyakazi bora ambaye yeye baada ya kukamilisha michoro mipango na kujenga daraja la Umoja. Wakati huo Mhandisi Mfugale alikuwa anasimamia barabara za vijijini na Marehemu Mhandisi Mjungi alikuwa anasimamia Wakala wa Barabara Tanzania.

Akitoa angalizo Rais ameagiza kuwa, daraja la Mfugale la Flyover la TAZARA lifungwe kamera mara moja hatutaki tuone watu wanakufa hapa tunataka yeyote atakaye sababisha ajali ajulikane.

Amesisitiza Mfugale hakupendelewa ni haki yake ametanguliza Utanzania badala ya masilahi yake binafsi Rais amesema kuwa nitawapa Mfano mmoja Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipendkeza kujenga umeme wa Stigler’s Gorge 1975.

Serikali ya Awamu ya Tano tumetenga fedha kwa ajili ya mradi huo wa umeme, hapa Tanzania gharama ya umeme ni kubwa mno ambayo kwa Unit moja ni 10.7 wakati Marakeni umeme Unit moja ni senti 0.12 Dolla za Marekani na Uingereza unit moja 0.15. Kama umeme wetu ni ghali ni kwamba hatuwezi kushindana katika soko la viwanda

“Hivyo, hatuwezi kushindana na wenzetu kwa kuwa gharama za uzalishaji kwao katika viwanda itakuwa ndogo, bila kuwa na umeme wa uhakika Tanzania ya Viwanda itakuwa ndoto”.

Wataalamu wetu wajue wamesomeshwa kwa ajili ya Watanzania ni lazima tujenge masilahi ya nchi yetu tusitumie utaalamu wa kukwamisha miradi yetu. Tujifunze sisi watanzania tufanye kwa manufaa ya Watanzania, lazima tuweke masilahi ya nchi yetu.

Akishukuru Serikali ya Japan Rais Magufuli amesema kuwa naomba ndugu zangu Watanzania tulitumie vizuri daraja hili, ili wenzetu wa Japan waone tunadhamii kazi yao. Pia nawaomba Japan washughulikie Flyover ya Gerezani imekaa muda mrefu tangu mwaka 2008.

Akiongeza amesema pia wafirkirie maombi yetu ya kuweka barabara za pete za (ring road) za Jiji la Dodoma ambazo tuliwaomba wazishughulikie ahakikishe anapokwenda Japan afikishe salam zetu hizo ili kuhakikisha kazi tuliyokusudia inafanyika

Mwisho kabisa Rais aimalizia kwa kutoa Ahadi ya kufanya ziara katika Jiji la Dar-es-salaam, pia, najua kuna maeneo mengi ambayo natakiwa kuyatenbelea.

Uzinduzi wa daraja la Mfugale Flyover TAZARA , umehudhuriwa na Balozi wa Japan anayemaliza muda wake wa Masahal Yoshima, Muwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan- JICA Toshio Magase, Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kuandikwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi.

Daraja hilo liliwekwa jiwe la msingi tarehe 16mwezi Juni 2016 na kuahidi kumalizika mwezi Oktoba tarehe 30, 2018, lakini limewahi kukamilika kwa takriban mwezi mmoja kabla.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi