Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Kutunuku Kamisheni kwa Maofisa Wapya wa Jeshi
Feb 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 03 Februari, 2018 atawatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Watakaotunukiwa kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.

Tukio la kutunuku kamisheni kwa maafisa hao litarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

02 Februari, 2018

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi