Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Azindua Mfumo Mpya wa Ukusanyaji Mapato
Jun 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_2279" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektroni (e-RCS) zilizofanyika Kijitonyama Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.[/caption]

  • Aagiza makampuni yote ya simu kujiunga katika mfumo huo

Na Jacquiline Mrisho 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameyaagiza makampuni ya mawasiliano ya simu kujiunga katika mfumo mpya wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) ya kusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (e-RCS) ili serikali iweze kupata kodi stahiki kwa mujibu wa sheria.

[caption id="attachment_2280" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Ukusanyaji Mapato  kwa Njia ya Kielektroni (e-RCS) zilizofanyika Kijitonyama Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.[/caption]

Rais Dkt. Rais ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama na baadae kuzindua mfumo wa ukusanyaji mapato kielektroniki uliotengenezwa na TRA na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

“Nimepata taarifa kuwa hadi sasa Kampuni za simu za TTCL, Hallotel na Smart ndizo pekee zilizojisajilikatika mfumo huu, sasa natoa wito kwa makampuni mengine na mabenki yahakikishe yanasajisajili kabla ya mwezi Desemba mwaka huu,” alisisitiza Dkt. Magufuli.

[caption id="attachment_2281" align="aligncenter" width="914"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akiwasili katika eneo maalum kwa ajili ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki (e-RCS) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2284" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ipad (Kishikwambi) atakayotumia kwa ajili ya kufuatilia Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato kwa Njia ya Kielekroniki kutoka kwa Mratibu wa Mfumo huo Bakari Mwangugu, katika hafla ya uzinduzi wa Mfumo huo zilizofanyika Kijitonyama Jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.[/caption]

Mbali na kujisajili katika mfumo wa (e-RCS) Rais Dkt. Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuzibana kampuni za simu ambazo hazijajiunga katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kujiunga haraka katika soko hilo kama sharia inavyozitaka.

Ili kuwezesha mfumo huo kufanya kazi, makampuni yote ya simu, mabenki na yale yanayofaanya miamala kwa njia ya kielektroniki yanapaswa kujisajili katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Kumbukumbu ambacho kina uwezo wakuona kila muamala unaofanyika na kufanya ukokotoziwa kodi inayostahili kulipwa.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli amezitaka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali kuacha kupoteza fedha kwa kujenga vituo vingine vya kutunzia taarifa na badala yake zitumie kituo hicho na pia kuboresha vile ambavyo tayari vimejengwa

[caption id="attachment_2287" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akibonyeza kitufe tayari kwa uzinduzi wa Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa njia ya Kielektroni (e-RCS) zilizofanyika Kijitonyama Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.[/caption] [caption id="attachment_2288" align="aligncenter" width="1000"] Ukurasa rasmi wa Rais ulioundwa mahususi kwa ajili ya ufuatiliaji wa Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato kwa Njia ya Kielektroniki (e-RCS) kama unavyoonekana mara baada ya kuzinduiliwa rasmi kwa mfumo huo leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kwa upande wake Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Shein amesema kuwa Serikali zilizo makini haziwezi kuwa na maendeleo bila kukusanya mapato hivyo wananchi wanatakiwa kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ili kujenga uchumi wa nchi ulio imara.

Nae Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Charles Kichere amesema kuwa mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji kodi unalenga kupata taarifa sahihi za mlipakodi na mtoa huduma ili kila mwananchi aweze kupata kiwango stahiki katika ulipaji kodi.

[caption id="attachment_2293" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akipeana mkono na Mratibu wa Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato kwa Njia ya Kielektroniki Bakari Mwangugu mara baada ya kuzindua rasmi mfumo huo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.[/caption] [caption id="attachment_2294" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wadau wa kodi wakifuatilia uzinduzi wa Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato kwa Njia ya Kielektroniki leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

“Hapo mwanzo kabla ya mfumo huu kuanza kulikua na changamoto mbali mbali kwani utaratibu ulikuwa ni wa mtu mwenyewe kujikadiria lakini kwa sasa mfumo huu utaboresha ushirikiano na utaondoa changamoto hizo na tunatumaini mfumo huu utaongeza ukusanyaji wa mapato,” alisema Kichere.

Baada ya uzinduzi huo, Rais Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein walikabidhiwa kishkwambi (Ipad) kila mmoja kwa ajili ya kuangalia mapato na kodi zote zinazokusanywa kupitia mfumo huo popote pale wanapokuwepo.

[caption id="attachment_2295" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Wakuu wa Kampuni za Simu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya Kielektroniki leo Jijini Dar es Salaam. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais UTUMISHI, Angella Kairuki, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles E Kichere. (Picha zote na: Frank Shija)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi