Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli awatunuku Kamisheni Maafisa wa Jeshi
Jul 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33396" align="aligncenter" width="873"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wakufunzi  baada ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018
[/caption]

Na. Immaculate Makilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi  Mkuu Dkt. John  Pombe Magufuli  amewatunuku Kamisheni  Maafisa  wapya 123 wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) katika cheo ha Luteni UsO.

Rais Magufuli amewatunuku Kamisheni Maafisa hao wapya wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu  ambao walikuwa wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi, kilichopo Monduli Arusha leo  [Jumamosi Julai 7, 2018] katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.

[caption id="attachment_33397" align="aligncenter" width="873"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi wakuu wa jeshi wastaafu kutoka kushoto Jenerali Hagai Mirisho Sarakikya, Jenerali Robert Mboma na Luteni Jenerali Tumainieli Kiwelu baada ya hafla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 7, 2018[/caption] [caption id="attachment_33398" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) aliowatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 7, 2018[/caption]

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho, Luteni Generali Paul Massao  Maafisa waliohitimu kozi ya 63 mwaka 2017 jumla yao ni 123 kati yao 118 ni watanzania,  na wahitimu 5 kutoka nchi za Uganda,  eSwatini, na Rwanda.

“Kati ya Maafisa  watanzania 118  wanawake ni 3 na wanaume 115, ambapo Maafisa 121 walipata mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Mondulu  na Maafisa wa 2 walipata mafunzo yao nchini India” alifafanua Luteni Generali Massao.

[caption id="attachment_33399" align="aligncenter" width="873"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mafunzo wakati wa hafla ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 7, 2018[/caption]

Sambamba na kuwatunuku Kamisheni Maafisa hao kwa cheo cha Luteni Usu, Rais Magufuli ametoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri ambao ni Emmanuel Kakuba Afisa aliyefanya vizuri zaidi darasani, Danie Meshack aliyefanya vizuri zaidi kwenye mafunzo, na katika medani ni Ramadhan Kakombe.

Wengine, ni Amstrong Mwamwesige kutoka Uganda aliyefanya vizuri kutoka nchi rafiki pamoja na Beatrice Kipinge ambaye ni mwanamke aliyefanya vizuri zaidi.

[caption id="attachment_33400" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 7, 2018[/caption]

Aidha, wahitimu 87 waliachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa, utovu wa nidhamu ama mtu kuomba kwa hiari yake.

Hafla hiyo ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wa ilipambwa na burudani kutoka vikundi mbalimbali ikiwemo kikundi cha ngoma za asili pamoja na kikundi cha mziki wa dansi cha Jeshi cha Mondulu jijini Arusha.

Aidha, tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2015  hii ni mara ya 6 ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwatunuku Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Ulinzi na Wananchi Tanzania (JWTZ).

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi