Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Atoa Mkono wa Idd kwa Watoto Yatima wa Kituo cha Malaika Kids
Jun 24, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4276" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga leo.Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abdullrahaman Mdimu na Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya.(Picha na: Frank Shija)[/caption] [caption id="attachment_4277" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdullrahaman Mdimu akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga leo. Mhe. Rais ametoa zawadi ya mchele kilo 150, mbuzi pamoja na mafuta ya kupikia ndoo mbili.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Mohamed Magati, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto H.Sanga na Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya.[/caption] [caption id="attachment_4278" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akimkabidhi zawadi ya shilingi elfu kumi mmoja wa watoto wanaolelea katika Kituo cha Malaika Kids wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kilichopo Mkuranga leo. Mtoto huyo amepewa zawadi hiyo kufuatia kujibu swali la Mkuu wa Wilaya huyo lililotaka kufahamu watoto hao wanataka kuwa wakina nani katika maisha yao ambapo mtoto huyo alisema anataka kuwa Rais. Anayeshuhudia ni Meneja maarufu kama Baba Mlezi wa Kituo hicho James Kallinga.[/caption] [caption id="attachment_4282" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo. Mhe. Rais ametoa zawadi ya mchele kilo 150, mbuzi pamoja na mafuta ya kupikia ndoo mbili.[/caption] [caption id="attachment_4285" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Kituo cha Kulelea watoto cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga, Pwani James Kallinga akitoa neon la shukrani kwa niaba ya watoto wa kituo hiyo mara baada ya kukabidhiwa zawadi za Idd El Fitri zilizotolewa na na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kituo hicho leo. Kutoka kulia ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdullrahaman Mdimu, Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga.[/caption] [caption id="attachment_4286" align="aligncenter" width="750"] Haya ndiyo baadhi ya majengo ya Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo wilayani Mkuranga, ambacho Mhe. Rais ametoa zawadi ya Idd El Fitri kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo hiki ambapo mpaka sasa kina jumla ya watoto 70 wanaolelewa wakiwa kituoni hapo (Picha zote na: Frank Shija)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi