Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Atekeleza Ahadi ya Milioni 60 kwa Waliohudhuria Mkutano wa CWT.
Dec 15, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24980" align="aligncenter" width="750"] Katibu wa Rais Ngusa Samike akikabidhi kiasi cha Shilingi milioni 60 kwa Kaimu Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa hapo jana mara baada ya kuendesha harambee ya papo kwa papo ambapo kiasi hicho cha fedha kilipatikana.[/caption] [caption id="attachment_24982" align="aligncenter" width="750"] Katibu wa Rais Ngusa Samike akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hicho cha Shilingi milioni 60 kwa Kaimu rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya. Katika fedha hizo, kiasi cha Shilingi milioni 50 zitagawiwa kwa wajumbe wote wa CWT waliopo mkutanoni na kiasi cha Shilingi milioni 10 ni kwa ajili ya wanafunzi Tarajali wa UDOM waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo.[/caption] [caption id="attachment_24983" align="aligncenter" width="750"] Fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 60 zilizo kabidhiwa kwa CWT ambazo Rais Dkt. John Pombe Magufuli alizichangisha kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa CWT siku ya jana. Katika fedha hizo Rais Dkt. Magufuli alitoa kiasi cha Tsh. Milioni 10 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa kiasi cha Sh. Milioni 10 pia na zilizobaki zilichangwa na viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo. Picha na Ikulu[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi