Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Amteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
May 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

TAARIFA KWA UMMA.

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Uteuzi wa Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza leo tarehe 22 Mei, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

22 Mei, 2017

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi