Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Ampa Tano Waziri Biteko
Nov 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Tito Mselem Bukombe,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli amempongeza Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe kwa kazi nzuri za maendeleo anazozifanya katika kuleta maendeleo jimboni humo.

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi akielekea mapumzikoni Wilayani Chato ambapo alisimamisha msafala wake ili awasalimie wananchi wa Jimbo la Bukombe.

Rais Magufuli amesema anawashukuru sana wananchi wa Bukombe kwa kumchagua Mbunge wa Jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa anamsaidia sana katika kutekeleza majukumu yake.

Aidha, Rais Magufuli amewataka wananchi wa Bukombe kuendelea kushirikiana na viongozi wa eneo hilo ambapo amesema amemchagua Biteko kuwa Waziri wa Madini ili atatue migogoro iliyodumu kwa muda mrefu.

“Naomba nichukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa Bukombe kwa kunichagulia Mbunge huyu, maana ananisaidia sana katika kutimiza majukumu yangu, nawapongeza sana,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameeleza kwamba, amemchagua Waziri Biteko kwenye Wizara ambayo inachangamoto nyingi katika ukusanyaji wa mapato ambapo kwasasa anaona muelekeo mzuri katika sekta hiyo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchi kuto kopa mikopo Bank ili wafanye miradi ya maendeleo, kwayeyote atakaye kopa ajiandae kuondoka madarakani.

Kwa upande wake Mbunge wa Bukombe ambae pia ni Waziri wa Madini Doto Biteko amempongeza Rais Magufuli kwa mradi wa Barabara ambapo Rais Magufuli ameongeza mtandao huo kutoka kilometa 256 za lami mpaka kufikia kilometa 1480 na miradi tisa mikubwa ya maji aliyotekelezwa na Rais wa awamu ya tano.

Pia, Waziri Biteko amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa wananchi eneo la kulima na kuchungia mifago yao ambapo sehemu hizo zilikuwa hifadhi ya taifa.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Biteko amemuomba Rais Magufuli kuangalia uwezekano wa kuongeza mtandao wa barabara kutoka Ushirombo mpaka Katoro.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi