Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Brig. Jen Dkt. Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (Medical Stores Department - MSD).
Uteuzi wa Brig. Jen Dkt. Mhidize unaanza mara moja, leo tarehe 03 Mei, 2020.
Kabla ya uteuzi huo, Brig. Jen Dkt. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Brig. Jen Dkt. Mhidize anachukua nafasi ya Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
03 Mei, 2020