Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Kikwete arejea nyumbani baada ya ziara ya siku moja nchini Rwanda
Mar 09, 2015
Na Mhariri

[caption id="attachment_124" align="aligncenter" width="3000"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikoalikwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikoalikwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.[/caption] [caption id="attachment_125" align="aligncenter" width="3000"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki[/caption]  

Wakati akiwa Kigali, miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete ameudhuria mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 

Mkutano wa leo ​pia umehudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zili​alikwa kuhudhuria mkutano huo. 

Mkutano huo ni ulijadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.

[caption id="attachment_126" align="aligncenter" width="1156"]Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects) katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects) katika Hoteli ya Serena mjini Kigali.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi